Fellowship - Lesson 04 - The basis of unity

Swahili

USHIRIKA KANISA NI NINI?

SOMO LA 4: MSINGI WA UMOJA

TAMKO LA B.A.S.F

Wakati Injili ilipo hubiriwa nchini Tanzania kwa mara ya kwanza, ilikuwa ni rahisi sana kupenda na kulinda umoja. Kila mmoja alimfahamu mwenzake jina lake, walifahamu mazingira ya kila mwamini. Walifahamu uwezo na ufahamu wa kila mmoja na walifahamu udhaifu wa kila mmoja.Walifahamuimani kila mmoja. Ni rahisi kuwa na umoja wakati wanapokuwepo wachache wa kuungana.

Lakini kadri idadi ilivyozidi kuongezeka, ndipo jambo hili likawa gumu zaidi. Kufikia mwaka 2018 sasa likawa ni ambo lisilowezekana kabisa, na kwa kweli, jumuia ya Wakristadelfia ilikuwa inafikia kilele cha hatari cha kuvunjika – ambapo haikuwezekana tena kuunganisha kila mmoja; palikuwa na hatari ya wazi ya jumuia kusambaratika.

Kitendo hiki siyo kwamba ni jambo jipya katika watu wa Mungu. Kwa kweli jambo kama hili lilitokea kwenye makanisa mengi nchini Tanzania, na tendo linalofanana na hilo lilitokea katika wakati wa kuanzisha Ukristo (Kristadephiani) duniani kote (ikiwemo Uingereza, Marekani na Australia). Ilitakiwa jambo fulani lifanyike ili kuwaunganisha.

Nchini Uingereza katika mwaka 1871 Ekklesia ya Birmingham walitengeneza tamko lililoitwa: “Tamko la Imani moja” ambalo ndiyo lililosababisha kuanzishwa kwa Ekklesia ya Wakristadelphia wa Birimingham. Waraka uliunganisha Ekklesia iliyokuwa na waumini wapatao karibu 1000.

19

Tamko la “Imani moja” ambalo ndiyo lililosababisha kuanzishwa kwa Ekklesia ya Wakristadelphia wa Birimingham; pamoja na Mafundisho ya uzushi (uongo) yanayofundishwa katika madhehebu siku hizi ulimwenguni, ambayo yanatakiwa yakataliwe na mwamini yeyote ambaye anapenda kuwa mshirika katika Ekklesia.

SEHEMU YA KWANZA – UKWELI WA KUAMINIWA.

Kwenye mkutano maalumu siku ya Alhamisi 22, July, 1886, hili tamko la Imani lilikubaliwa na Ekklesia zote za Wakristadelfia duniani kote kuwa Tamko kuhusu Imani la Birmingham. Mabadiliko madogo yalifanyika siku ya 14, Septemba, 1908, na kuwa na nakala iliyosahihishwa tarehe 10, Septemba, 1968, na nakala hii ilijulikana kama “Tamko la marekebisho kuhusu Imani la Birimngham” au B.A.S.F. kama inavyofupishwa, ingawaje jitihada ya kuwapatia nakala hii katika Tanzania yalifanyika kabla, lakini ilikuwa siku ya 16, Februari, 2019, ambapo tamko hili lilikubaliwa na Ekklesia ya Tanzania.

Ni kwa nini hati hii ni ya muhimu sana? Ni hakika kuwa umoja wetu unaotokana na imani na kuifuata Biblia. Ndani ya Biblia ndimo ilimo hati yetu ya umoja wetu. Wakati huo ni ndiyo ukweli, Maandiko Matakatifu yenyewe yako wazi kufasiriwa. B.A.S.F. Ni dhahiri kuwa inaeleza mafundisho ambayo Wakristadelfia wanayaamini na kuna mafundisho ya uzushi (uongo) yanayofundishwa na madhehebu ambayo Wakristadelphia wanayakataa.

Ndugu wanaume na wanawake ambao hawaamini na hawafuati hii B.A.S.F. hukataliwa katika ushirika wa Jumuiya ya Wakristadelfia. Na siyo tu kuwa huondolewa kushiriki mkate na divai,pia watatakiwa kuachilia huduma walizo nazo ( na hata kwa nguvu ikilazimu )ambazo walikuwa wakihudumu; nao watachukuliwa kama ndiyo “kwanza wanajifunza mafundisho, ili wabatizwe kama watakuwa wameelewa” – na katika mazingira mengine huondolewa katika Ushirika.

Kuwa na umoja ni muhimu katika ushirika wetu.

Nafasi ya juu ya heshima sana.

Tumepata nafasi ya heshima sana kutokana na maarifa ya ufunuo wa kusudi la Mungu. Watu wengi wenye juhudi ya dini bado wako gizani kuhusu kweli ya Mungu. Kwa ajili ya heshima hii tuna deni kubwa mno kutokana na ukweli kuwa kwa kudra yake Mungu, Daktari Thomas alifanyika chombo muhimu sana kwa kuirejesha Injili kama iliyokuwa mwanzo kutoka kwenye mapokeo ya ukristo.

Mapokeo hayo yalikuwa yameenea akilini mwa watu yakiwa ni matokeo ya uharibifu wa walimu maarufu ambao waliyadharau yaliyo ya kweli juu ya Mungu, kwa kushika nadharia za kibinadamu. Daktari Thomas alirudi kwenye Neno la Mungu na matokeo yake ya kusoma sana na kuhojiana na watu hatimaye alipata Kweli. Tunapotafakari katika uhalisia ya kwamba Kweli imepotea na huku giza likizidi kuishinda (kutanda juu ya) nuru,ndipo sasa tunatambua umuhimu wa kusikiliza ushauri wa mtume kuhusu kushika sana Neno la uzima ambalo tuliambiwa.

Hatuwezi kusoma nyaraka bila kuwa na hisia ya dhati juu ya mateso yaliyowazunguka; nayo historia ya karne za mwanzoni inaonyesha jinsi Roho alivyowaongoza mitume yalewaliyoyanena na kuyatenda. Kwa zamu yetu sisi tunawajibika “kutunza na kuweka”, kama vile Paulo anavyobainisha ukweli katika waraka wake kwa Timotheo, kwamba ayatunze moyoni mwake, sawa na kuweka fedha mikononi mwa mmiliki wa benki, ni lazima itunzwe isipotee.

Je, ni umuhimu gani wa kuilinda Kweli iokoayo? Haya ya muhimu yameainishwa ndani katika Marekebisho ya Tamko la Imani la Birmingham.

Si kwamba matamko mengine hayangeweza kuwa ya kweli, lakini Tamko la Birmingham ndilo linalojulikana kwa upana zaidi. Ndilo linatambuliwa na wote ndani ya kile tunachokiita Ushirika wa Katikati. Katika Uingereza limekubaliwa na makundi yote ya Ekklesia huko Central na Suffolk street kwamba ndilo tamko ambalo wote wanapaswa kukubali kuwa ni Kanuni za Msingi wa Imani moja.

Tamko la Imani ni la msingi kwa kila jumuia ya waamini kuelezea imani yao ili kuhakikisha utendaji kazi wa pamoja na shuhuda zenye mtiririko mmoja kwa watu walio nje. Kulidharau tamko kuwa limeundwa na wanadamu na kusema kuwa Biblia peke yake ndiyo kamilifu inadhihirisha kushindwa kuelewa matatizo ya maisha ndani ya jumuiya ya Ndugu katika Kristo na kazi zake.

Madhehebu yote yanayodai kuwa imani yao inategemea Biblia, ukweli wenyewe ni kwamba wanaonekana kabisa kuwa wanahitaji Tamko la kile tunachokielewa kuwa ni fundisho la Neno la Mungu. Ekklesia katika Australia, Marekani na kwingine kote pia, wanatumia Marekebisho ya Tamko la Imani la Birmingham; kuwa kielelezo cha umoja wa Imani inayowaunganisha waamini wote. Tunawaagiza ninyi hili mlizingatie kwa dhati.

Majukumu na wajibu

Kuna majukumu na wajibu wa ndugu kwa ajili ya kusudi lililofunuliwa, majukumu ambayo huwa na mwonekano wa ndani na nje ya waamini. Mwonekano wa ndani — ni kwamba tunalo jukumu la kulisha akili za ndugu zetu kwa kuambia Injili, ili kuwajenga katika Imani, ili wakue katika upendo kati yetu na kuwa watiifu wa amri za Bwana. Lakini pia tuna kazi ya kuyapinga mafundisho yasiyo kuwa ya kweli. Jinsi nyaraka zilivyo nyingi katika Agano Jipya zilizo andikwa na Mitume katika kazi hii. Jinsi Paulo alivyotamani sana kuona watu alioamini mahubiri yake, ili waimarike katika maneno yale aliyowahubiri! Na ikiwa aliwafikiria waamini kuwa ni kondoo, pia aliwachukulia walimu wa uongo kuwa ni mbwa-mwitu ambao waliwala kondoo walio kundini.

Iwapo alifikiri kwa shukrani za dhati watu waaminifu waliofanya kazi pamoja naye kwa bidii, pia alisema kwa tahadhari kuhusu wale aliowaita mitume wa uongo. Tunafanya haya marejeleo pasipo kutumia lugha kwa kumtaja yeyote, ili kuweka fundisho la jukumu letu na wajibu wetu katika kundi. Tunao wajibu wa ndugu zetu katika Bwana huko Dar es salaam, Mbeya, Ninde au katika maeneo mengine yoyote. Wajibu huu ni wetu sisi katika Ekklesia yetu.

Tunalazimika kuwa na haki ya kuamua kuhusu nyadhifa za waamini wenzetu, pamoja na madhaifu yao, na mambo ya desturi ya mtu binafsi na wakati wa tuhuma yanapokuwepo kila Ekklesia wanatakiwa kufanya uamuzi. Wakati jambo hili ni jukumu letu (na ni lazima tuhakikishe kuwa hakuna yeyote anayetuondolea jukumu letu hili) maana tunawajibika pia kwa ekklesia zingine. Wakati kila ekklesia, ni sehemu ya Ekklesia moja— yaani mwili wa Kristo, na wajibu wetu kwa Ekklesia zingine ni kuendelea kuitunza Kweli na kuiruhusu nuru iangaze katika giza liletwalo na mawazo mabaya.

Lakini kinyume chake ni masikitiko hakika— iwapo Ekklesia kwa makusudi tu na wanaendelea kuhubiri makosa, inawezekanaje kukwepa majukumuu yetu, isipokuwa tuwe tumekataa uhusiano? Na kama msingi huu kwa wakati fulani unakandamizwa mno,basi inatulazimu, katika hilo,kufuata njia nzuri ya amani ili kulishughulikia. Kwa maana ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha unakuwepo Umoja. Tunapaswa tuepuke jambo lolote linaloondoa umoja, mabishano, matusi na ugomvi wa maneno. Kwa kuwa Umoja ni umoja wa imani, basi hilo linahusu mapatano katika mambo yaliyo ya muhimu.

Hapa inawezekana tunaweza kuruhusiwa kusema wazi wazi. Katika juhudi zetu za kutafuta umoja na amani katika nchi ya Uingereza, ndugu katika nchi za nje wametukumbusha sisi kwa njia tofauti tofauti kuhusu matatizo yanayoendelea kuwepo katika nchi zingine ambako bado matatizo yanaendelea,yakizidishwa sana na uhasama wa tofauti za maeneo yao. Kama tuna jukumu la kukwepa kuweka vikwazo katika njia yenu, je, ninyi ni jukumu lenu kutenda kunyume chake na hamtasaidiana kuweka vikwazo vya hatari kwa umoja, moja wapo ni sawa kwa kuwafundisha waamini wenu kwamba mnaweza kwa furaha mkatamka kuwa kuna umoja wa Imani moja, au kumwondoa kwenye ushirika wenu, hata kama ni jambo la kusikitisha kulitenda, huyo anayefundisha makosa. “Ondoeni chachu ya kale”, ndiyo ushauri wa Mitume.

Hisia mbaya

Kwa hiyo katika kuzingatia wazo hili, tunapenda kusema wazi wazi hatutaweza “kusema kuwa mtu ni mkosaji kwa ajili ya neno”. Tunapaswa tujiepushe na hila yenye maneno yanayotumiwa sana lakini mara nyingi hayafafanui ukweli halisi wa neno lile. Tunatakiwa tutenganishe kati ya kanuni za kweli za maneno na maneno ya misimu yasiyoeleza ukweli wa maneno. Maneno ya misimu ni maneno hatari sana, kwa kuwa yameibuka katika lugha kwa kipindi fulani na yanamtumiwa na jamii ,hadi jamii inasahau yalitokea wapi . Maneno ya misimu yameingizwa katika lugha na yanatumika katika tafsiri rasmi ya lugha. Hisia mbaya hulikuza jamba baya kuwa baya zaidi na huzuia uelewa wa halisi wa jambo hilo. Kufanya matatizo kuwa makubwa dunia ni ni sawa na kusambaza ugonjwa wa kifua kikuu au kansa ,matatizo ya sehemu tiba yake ni kulishughulikia kwa uaminifu katika eneo husika na kama ni Ekklesia basi inatakiwa wajulishwe, na haki kama ilivyo kanuni ya sheria, basi ule uamuzi ni lazima usiwe tu wa haki bali uonekane kuwa wenye haki, kwa hiyo katika kutengana isiwe tu ya maandiko na uaminifu kwa amri za BWANA(Yahwe) bali ni lazima ionekane kuwa ni uamuzi wa hakika na kweli. Kwa hiyo uamuzi uonekane ku wa ni wa hekima na busara.

Tunaamini kuwa kuna mamia ya ndugu waliotengwa kutokana na matokeo ya kukoseshwa na walimu waliowafundisha , au ambao kwa mwenendo wao na maneno ya mafundisho yao yamekuwa dhahiri kuwa walifundisha makosa. Wajibu muhimu umejikita juu ya jambo hili. Lakini inatupasa sisi sote kuondoa vikwazo na vizuizi katika njia ya wale watu ambao kwa nia moja waliotengwa kutokana na makosa ambayo hawakuyafanya wao.

Inatupasa kuwatafuta wale ambao wamepotea na (ikiwezekana) tuwarudishe tena katika zizi. Na pale inapowezekana kwa nia nzuri ya ufafanuzi kuhusu mjadala wa mafundisho ya imani,basi maneno mazuri ya Mungu ndiyo yatumike, maneno rahisi ndiyo yanayotakiwa pia yatumike na kuweka kanuni za msingi ili zifuatwe.


 

Kwa hiyo tunachukua nafasi hii kuwaomba ushirikiano katika kuitafuta amani na umoja kwa wale wenye nia moja ya Kristo. Maana, kama BWANA, Mungu asingekuwa mvumilivu akalirudi kusanyiko lake la karne ya kwanza kwa sababu walishika mafundisho yaliyo mchukiza au angewatesa wale walioshika mafundisho hayo, basi,tunaona ni jinsi gani mambo yangechukuliwa kwa uzito wa juu; ni hakika kuwa hakuna mtu miongoni mwetu angekuwa katika nafasi hii kama Mungu angetuangalia katika jicho lile

Na kwa sababu hiyo, tunasikia habari za watu wanaopinga imani yetu katika Kristo na wakiidhihaki pia imani yetu ,na sasa tunawaombeni ninyi mtusaidie ama kwa kuwatenga hao ndugu waletao matengano na migawanyiko kwa maneno yao, au kwa kuwaonyesha (baada ya utafiti) kwamba tuhuma zilizotolewa dhidi yao hazikuwa za kweli. Tunajisikia kuwa na uhakika wote kufanya hayo mtasaidia sana kuieneza Kweli ulimwenguni pote na kazi ya amani katika Ekklesia zote nchini na duniani pia.

.Katika mwaka 1900

Katika mwaka 1900, akiwa katika ziara ya kutembelea England na Wales, Ndugu Thomas Williams aliandika “kipindi cha kujenga”, akigusia “hali ya kugawanyika kwa ndugu katika visiwa vya Uingereza”. Ndugu Williams aliwapa changamoto ndugu wa Uingereza kuitafuta amani, ili kuacha migogoro ya kusisimu-nywele na kuweka msimamo kwenye “Tamko la zamani la Birmingham la Imani ya Wakristadelphiani,” ambalo alipendekeza libadilike jina na kuitwa “Tamko la Imani ya Wakristadelfia, na hivyo kumaliza uhusiano na majina ya sehemu. Wakati ule Ndugu William alitamka, “Ndugu huko Amerika walifanikiwa katika kuondoa uchungu wa matatizo haya ndani ya mioyo yao…” Huko Marekani walitaabika sana kwa kuwa baadhi ya waamini walifanya kinyume kwa mfano unaofanana na haya tunayo yaona Tanzania leo. Hakuna jambo lolote jipya katika mambo haya. Ni tabia ya mwilini. Hata hivyo mambo mengi yamefanyika katika Ekklesia huko Amerika katika miaka ya 119 tangu Ndugu Williams alipoandika ombi lake.

Mfano ni matatizo ya Marekani

Mambo mengi ya mashindano na migawanyiko katika Jumuiya ya Marekani ilihusisha uelewa tofauti katika tofauti ya imani zilizoshikwa na jumuia za Wakristadelfia wengine, pamoja na tofauti zilizohusu mahusiano na uwajibikaji kwa wale walioshiriki aina tofauti za ujuzi katika ufahamu kati ya Wakristadelfia. Katika mashauri mengi ilikuwa kuelewa dhamiri,kinyume na mambo muhimu ya imani zilizoleta mitafaruku mingi ya kukatisha tamaa” katika jumuia iliyokuwa haijakumbwa na tatizo kama hili; na ni katika maeneo kama haya ndugu wa Tanzania inawapasa kuenenda kwa uangalifu na kwa upendo wa ndugu ili kukabiliana na tofauti inayowakabili.

 

Hii haina maana kwamba mafundisho potofu au mwenendo wa dhambi unakubalika, wala hatuwezi kukumbatia mahusiano ya hovyo ya kijamii kwa gharama ya imani yetu na uwezo wetu wa kuyahubiri, lakini utofauti katika kuelewa dhamiri nje ya misingi ya imani isiwe ndiyo chanzo cha chuki na tafaruku katika Ekklesia. Sala zizingatie mwongozo kwa ndugu katika kukabiliana na kusuluhisha mambo ambayo mara nyingi huleta utata, na kukiwa na tahadhari maalumu ya kuzingatia amri za Kristo na kanuni za ushiriki.

Amri ya Kristo

“Maagizo ya Kristo” yanapatikana katika B.A.S.F. tangu wakati wa mwanzo wa karne ya 20. Kutokea kwa amri hizo kunatoa ukumbusho unaosaidia tabia na mwenendo ambao tunatazamiwa kujibia kwenye kiti cha hukumu. Kuhusu wajibu wetu kwa ndugu, tunakumbushwa kuwa“msinung’uniakiane, msihukumu…msilaumiane” na “uchungu wote, na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu”. Na zaidi ya hayo yote kwa ajili ya mahusiano kati ya ndugu, Kristo alisema, “Hii ndiyo amri yangu, pendaneni kama na mimi nilivyowapenda ninyi”.

Maonyo kwa ajili ya mifano ya upendo wa ndugu yameandikwa kila sehemu katika Maandiko, na ndugu wote wanakiri na kufuata kwa uzuri na umuhimu wa tumaini hili. Wakati matatizo yanapotokea inatakiwa tujihadhari na mwili, hasira na uchungu mioyoni unaozaa hasira na ugomvi.

Ikiwa dhamiri itamwongoza mtu kutoafiki jambo fulani, kuonya, au kujitenga katika ushiriki kwenye shughuli maalum za Ekklesia au kujiondoa kabisa katika Ekklesia yenyewe, ni jambo muhimu sana tukutane na makundi yote mawili ili kufahamu jambo lililomtia uchungu au kumchukiza na kutokusamehe na kumwonyesha upendo huyu ndugu na tukubaliane wote. Mihemuko ya mwili na kughadhabika ni hali za kawaida kwa wote, ndipo inapotakiwa kuchunguza kwa kina ili ukweli ujulikane kwetu sisi na kwa ndugu yetu. Tuzingatie kwamba tumeagizwa kuwapenda adui zetu, je, siyo zaidi sana kuwapenda na kuwabariki na kuwaombea ndugu zetu?

Nabii Amosi, anauliza “Je, watu wawili wanaweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” Ushirika ni zaidi ya Meza ya Bwana (yaani tendo la kumega mkate na kunywa divai). Ushirika unahusu mambo yote yanayo takiwa kuzingatiwa “kwa pamoja”, naye Yohana anashuhudia mafundisho haya (" Lile tulilolisikia, na tuliloliona kwa macho yetu "), na kutembea vilevile (“tukitembea nuruni”) na ndiyo ushirikiano wetu. (1Yohana 1:3-7). Ingawaje kuna “uhuru” ndani ya Kristo, lakini uhuru huo unakuwepo pale tu penye msingi na mipaka ya amri zilizowekwa kwa ajili ya kutufundisha.

Dhamiri ni lazima iongoze uhuru huo, lakini uhuru unabakia katika mipaka iliyotajwa, damiri isisababishe kukosa. Paulo anauliza “kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine, maana ninyi “ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuutafuta mwili, basi tumikianeni kwa upendo. Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.

Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana… Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. “

 

Jumuia ya Tanzania ni dhahiri ya kuwa Kweli ipo njia panda

Jumuia yetu ni dhaifu nayo inayofuata nia ya mwili na tabia za mwilini ambazo zinahatarisha uhai wetu kama ndugu katika Kristo na hata kudumu kwetu tukiwa jumuia ya Ekklesia. Hata maono yetu ya umojo wetu kama familia haikumbatiwi na kila mmoja,lakini hakika amani na nia njema kati ya ndugu, inayosimama kwenye msingi wa ujuzi wa imani moja yenye thamani, utakubalika . Kurudi kwa Bwana wetu ni kumekaribia.

Inatupasa wote kwa pamoja tuimarike katika katika kweli na kusonga mbele kwa pamoja kwa jinsi tunavyoweza, tuimarishane na kutiana moyo wote watu binafsi na Ekklesia zetu; tutupilie mbali “uchungu wote, na hasira … na matukano” kila tupatapo nafasi. Na kila mmoja wetu anaweza kuchangia katika kutibu mifarakano iliyopo ndani ya Ekklesia zetu na katika jumuia kwa njia ya maneno yetu na matendo. Tumebarikiwa kuifahamu na kuidumisha ile kweli, na ni kwa tunashirikiana ufahamu huu, kama inavyowakilishwa katika Tamko la Imani, ambalo linatuhimiza kuweka lengo la juhudi yetu “kutunza umoja wa Roho katika kifungo cha amani” (Waefeso 4:1-4).

Tutahitimisha kwa sala ili Mungu abariki juhudi zetu za pamoja kwa sifa za Jina lake, kwa kuinua mioyo ya watakatifu wake, na kuwaunganisha pamoja wote, ambao wana amini ahadi za thamani kubwa mno za Mungu, na wanatazamia Ukombozi utakaoletwa na Bwana atakaporudi tena. Baraka za Mungu ziwe juu ya mkusanyiko wenu hadi mwisho

Swahili Title
Ushirika - Somo la 04 - Msingi wa Umoja
Swahili Word file
Literature type
Sub type
English only