ARUSI YA KANA - Mwujiza wa kwanza wa Yesu

Swahili

ARUSI YA KANA

 Mwujiza wa kwanza wa Yesu

Somo: Yohana 2:1-11

Mtume Yohana aliandika miujiza nane, ingawaje hakuielezea kuwa miujiza, lakini aliitaja kuwa ni ishara. Ni neno ambalo lina maana ya “nguvu”, lililotumiwa mara nyingi na waandishi wengine wa Injili kuelezea miujiza, ila Yohana hakulitumia neno hili. Ni mara moja tu neno lililofasiriwa kuwa ni “mwujiza” linapatikana katika Injili iliyoandikwa na Yohana, lakini linafuatana na neno “ishara”. Lakini neno ambalo limetafisiriwa “ishara” limeonekana mara kumi na saba.

Utaratibu wa Yohana wa  kutaarifu  husababisha kuelezea moja kwa moja: anasema kuwa ni mwujiza wa kwanza, kuwa  “ mwanzo wa ishara”; na mwujiza unaofuata anauita kuwa ni “ishara ya pili”.  Mwujiza wa saba ( kwa kuhesabu kwangu) ulikuwa  ni ule wa kufufuka kwa Lazaro, na wakati huo huo  mwujiza wa nane na ambao   ndiyo ishara ya mwisho ilifanyika baada ya kufufuka kwa Kristo.

Kwa kuendelea kutumia neno “ishara” kuanzia mwanzo hadi mwisho, ni na amini kuwa Yohana anajaribu kutuonyesha ukweli halisi wa miujiza, ambayo ilifanyika kama ishara. Miujiza ili kuwa ni zaidi ya udhihirisho wa nguvu; kusudi lake kwetu ni kutuonesha ukuu na uweza wa Mungu zaidi. Miujiza ilikuwepo kama kiashirio kwetu kwa ajili ya uweza wa mambo makubwa.

Huu ulikuwa ni “mwanzo” – au “kwanza” – katika mfululizo wa miujiza ,Yohana aliyoiandika, ambayo ilitakiwa ifahamike kama “ishara” zinazounganika pamoja na kuwa ishara nne zinazo fuatana mfululizo wa kanuni ya Uungu ili Taifa la Israeli liweze kumrejea BWANA, ambayo ndiyo njia ya kweli ya kumtia moyo mtu wa Israeli wa kiroho katika mlango ule ambao ni mwembamba, na njia iwaongozao katika uzima wa milele.

Katika tendo hili sisi nasi tunahesabiwa haki kwa kutazamia maana iliyo kubwa zaidi katika miujiza iliyo andikwa. Kwa kweli tunaweza kwa urahisi kupata aina nyingi na ishara hizi zenye maana hasa ya miujiza hii yote ambayo tuna soma katika Maandiko Matakatifu.

Nguvu alizokuwa nazo Yesu, n ambayo ni nguvu za Roho Mtakatifu, alipewa na Mungu wakati alipobatizwa. Wanafunzi wake walikuwa bado kumwona akitumia nguvu hii. Walikuwa wameamini maneno ambayo Yohana aliwaambia, ya kuwa Yesu likuwa “ mwana kondoo wa Mungu” na wao walimfuata.Walisikiliza  maneno ya Yesu , wakawa wanafunzi wake; lakini walipoiona miujiza yake, ndipo walipoaminishwa kwa uthibitisho wa matendo ya uweza wa nguvu, na kuwa  ndiye alikuwa ni Kristo. Na pia ninafikiri kuwa uthibitisho mkuu mara nyingi ulitokana hasa na maana ya ujumbe wa miujiza ile.

 (Yohana 1:36)

KUISHIWA DIVAI:

Ilikuwa ni siku chache tu baada ya Yesu kukusanya wafuasi wake wa kwanza wachache, akaalikwa kwenye arusi katika Kana ya Galilaya

Yohana anabainisha kuwa, aliandika sura ya pili kwa kueleza sababu za msingi za kulinganisha mambo hayo mawili na sura mbili za mwanzo. Husianisho la kwanza, ni wakati anapofanya kuwa rejea “siku ya tatu”. Maana hii hasa ilikuwa ni siku ya saba ya taarifa ya Yohana .Na ilikuwa ni siku ya tatu baada ya Yohana 1:43

Namba tatu ni muhimu sana kwa kuwa ni lugha ya picha au ni namba yenye kuwakilisha maana katika Maandiko Matakatifu. Inazungumzia kuhusu ufufuo uliofanyika kupitia agano ambalo limethibitishwa kwa njia ya dhabihu. Namba tatu  ina uhusiano  kabisa na ufufuo  halisi wa Kristo   kama ilivyo kuwa imetabiriwa  tangu mwanzo na Mungu . Yesu, alikuwa ni mzaliwa wa kwanza kati ya wale watakaofufuliwa kwa ajili ya kupewa uzima wa milele. Kwa hiyo, namba tatu inafaa sana kama  alama  ya fumbo inayowakilisha ufufuo wa utukufu wa mwili wa Kristo,  mkutano mkubwa sana wa waamini ambao “watatukuzwa pamoja na Kristo” kwenye kiti cha hukumu

Na tukio hilo litakuwa ni sherehe ya arusi kubwa mno wakati wote, wakati Kristo na bibi arusi wake watakapohitimisha na kukamilisha hili unganiko.

 (Ufunuo. 19:7-8)

Maana hii hasa ilikuwa ni siku ya saba ya taarifa ya Yohana .Na ilikuwa ni siku ya tatu baada ya Yohana 1:43

Ukweli kuwa arusi ya Kana ilifanyika siku ya saba ya taarifa mfululizo za Yohana, inavutia kuhusu fundisho la kiroho; maana itakuwa ni siku ya  saba ya mwaka wa mika elfu moja,  baada ya siku ya sita ya mwaka wa elfu- moja  wa utawala wa dhambi, kwa kuwa  tukio  la kukamilika   kati ya Mwana kondoo na  bibi arusi  ndipo litakapofanyika.

Kana, iliku ni nyumbani kwa Nathanaeli. Mariamu, mama yake Yesu alikuwepo, na wanafunzi wa Yesu walikuwa wamealikwa pia. Familia mojawapo au familia zote mbili za arusi walikuwa ni marafiki au inawezekana walikuwa jamaa ya karibu, ya familia ya Yesu, kwa kuwa mama yake “alikuwepo pale”, hii ina maana kwamba, Mariamu alikuwa akiishi pale.

Uhuru wake katika kuwashauri wahudumu ili wafanye lolote atakalosema Yesu ni uthibitisho wa jambo hili. Yesu alialikwa; na Yohana anaeleza, kuwa “Yesu aliitwa, na wanafunzi wake”, anaelezea kwamba wanafunzi walialikwa kwa sababu ya uhusiano wao na Yesu.

Yusufu, mume wa Mariamu hatajwi, ni vigumu kuelezea kukosekana kwake katika tukio hili muhimu, isipokuwa tu, labda alikuwa tayari ameshafariki.

Neno la Kiyunani linalotumika kwa “kuitwa” ni Kaleo. Ni neno moja ambalo   mara nyingi limetumika katika Agano Jipya kuelezea mwaliko ambao Mungu anaendelea kuwaita wanaume na wanawake kwenye Injili.  Na pia, neno hili limetumika kuwakilisha wito wa Krito atakapo waalika wale watakaokuwa wamesitahili kuhudhuria karamu  ya mwana kondoo

(Ufunuo 19:9)

Si fikirii kama Bwana Yesu Kristo alilitumia tu neno linalofanana alipoelezea mfano kuhusu watu wale “walioalikwa kuja arusini.

(Mathayo 22:3), arusi kila wakati lilikuwa ni tukio la furaha. Na katika siku hizo sherehe na nderemo pamoja na familia na marafiki   ingeisha baada ya siku kadhaa. Wakati mwingine ingechukua siku saba, na wakati mwingine majuma mawili.

Kuna jambo lililotokea kwenye arusi hii ambalo lingeharibu furaha ya tukio zima na kusababisha huzuni kwa mwenyeji- divai ilitindika kabla ya sherehe kuisha.

Ni tukio ambalo kwa kawaida halitarajiwi kutokea la divai kutindika (kuisha) mapema – kwa kuwa ni bidhaa muhimu sana –   hata imalizike katika hatua za mwanzo kabisa za sherehe. Hapo kuna sababu moja tu  ya kuelezea: ambayo  ni kwamba watu  waliohusika  kuiendesha sherehe  ni masikini  hata wakashindwa  kuweka mahitaji maalumu kwa ajili yao wenyewe  au jamaa zao na marafiki wao.

Haya maelezo  ya kukosa divai ni  muhimu,na yanafaa sana, kwa kuwa  watu wale waliokusanyika arusini, ni ishara yenye maana halisi  ya Taifa la Israeli. Kwa hiyo kukosekana divai ikawa ni sababu kuu ya (muujiza) “ishara”.

Katika Maandiko Matakatifu, divai ilikuwa ikitumiwa mara nyingi kama alama ya mafundisho ya imani. Na pia huwakilisha damu, ambayo ni “uhai”. Kwa hiyo, katika “ishara” hii ya kukosa divai inawakilisha kukosa maisha ya kiroho.  Na hivi ndiyo ilivyo eleza kuwa Taifa la Isreali wakati Mwana wa Mungu alipokuwa akitembea katikati yao; alikuja ili kuwaondolea ukosefu wa maisha ya kiroho, ikiwa tu watu wa BWANA wangepokea mafundisho yake.

Na pasipo mashaka yoyote, “walikuwa ni kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli”.  Dini, kama inavyofahamika na kama taifa walivyotenda maovu wakati wote, walikuwa wameoza. Kwa  namna yoyote  kwamba walitambua vyema mahitaji yao muhimu au hawakutambua, watu hawa walikata tamaa kwa kukosa matumaini na wakataabika  wasiweze kujiokoa kutokana na uwezo wa “divai”  iliyo na  mafundisho ya uzima na yenye nuru iokoayo.  Na ni Mwana wa Mungu pekee ndiye angewapatia wao “divai” ya kiroho ambayo ingeweza kuwajaza na kuwatoshereza ili kuwarejezea nguvu za kiroho.

Lakini taifa la Israeli hawakusitahili kusimama mbele ya Mungu wao. Kwa kuwa “divai” , yaani mafundisho ambayo viongozi wao wa dini waliwafundisha  ili wayaamini, yalikuwa ni sawasawa na divai  ile  iliyoisha mwanzoni kabisa wa sherehe ya arusi.

Kusudi la ishara hii kwa taifa la Israeli ilikuwa kuwaonyesha kuwa  hawakuwa na matumaini ya kiroho, na kwamba ni Mwana wa Mungu tu , yaani Masiya wao, ndiye angeweza kuwapatia mahitaji yao ya kiroho na kuwarejeza kwa  BWANA.

Wakati Mariamu alipoiona aibu hii, ndipo akamwambia Yesu, " Hawana divai " (mstari 3).Yesu alifahamu mama yake  alitumaini kuwa  Yesu angeweza kuwasaidia akamwambia mama yake, “ Mama, tuna nini mimi nawe?” (mstari 4).Alihitaji mama yake atambue kuwa   jambo lolote ambalo angelitenda kuanzia muda huo na kuendelea, tangu alipobatizwa angefanya ili kumpendeza Mungu. Na ingawa Yesu alimpenda mama yake na alipenda kumpendeza, lakini alipaswa kuitenda kazi ya Baba yake tu. Kwa kuwa saa yake ilikuwa haijawadia ya kujidhihirisha mbele ya watu wote. Hata hivyo, alifanya muujiza wakati huu kuwa ishara kwa ajili ya wanafunzi wake na watu wale waliokuwa wamehudhuria kwenye arusi ili wafahamu kuwa yeye ndiye Krito.

 Mariamu alikuwa amejifunza kumgeukia mwanaye wakati wa shida. Mariamu   hakuwa na mashaka alikuwa na uzoefu  wa hekima aliyokuwa nayo Yesu   walipokuwa wanaishi kule Nazareti; lakini matokeo ya wakati huu, pamoja na maarifa aliyonayo Mariamu ya kumfahamu  ambaye ni Baba wa mwanaye, ndiyo hasa iliyomwongoza sasa kutarajia jambo ambalo ni kubwa zaidi, ya kuona baadhi ya matendo ya udhihirisho wa nguvu. Na jawabu la Yesu, alisema kuwaSaa yangu haijawadia”, inadhihirisha jambo hili.

  MAJI KUWA DIVAI  

Mariamu aliamini na kukubali kuwa Yesu atasaidia. Akawaambia watumishi, “Lo lote atakalowaambia, fanyeni” (mstari 5).

Kwa kuwa nje ya maingilio ya mlango wa nyumba kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko ili wageni wanawe mikono kabla ya kula, siyo kwa sababu wamechafuka, bali kwa desturi (mapokeo) ya Wayahudi ya kutawadha.(Marko 7:3-4)

Yesu akawaambia watumishi, “Jalizeni mabalasi maji".  Nao wakayajaliza hata juu, ndipo akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Huu ulionekana ni utaratibu mpya, lakini Mariamu alikuwa amewaambia mapema wafanye lolote ambalo angewambia. Lakini, walishangaa, walipoyateka- hayakuwa maji, ila ilikuwa divai iliyotoka katika yale mabalasi makubwa ambayo wao wenyewe walikuwa wameyajaza maji. Naye mkuu wa meza alipoionja ile divai, yule mkuu wa meza alimpatia mkono wa (tahania) pongezi bwana arusi kwa kuendelea kuwapatia divai iliyo njema.  Akamwambia, watu wengi kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; "lakini", wewe, “umeiweka divai iliyo njema hata sasa" (mstari10).

NI KWA NINI YESU ALITENDA MIUJIZA:  

Nguvu ya Mungu ni kubwa kuliko nguvu yoyote aliyo nayo mwanadamu. Utakumbuka jinsi Mungu alivyotuma mapigo kwa Farao na kwa watu wa Misri na hata wachawi wao nao wakajaribu kumwigiza Musa. Kwa ujanja wao, mapigo ya mwanzo walionekana kuyaweza, lakini hatimaye walikiri kuwa ilikuwa ni nguvu ya Mungu iliyokuwa ikifanya kazi kwa mikono ya Musa. Kwa hiyo katika miujiza aliyoifanya Yesu alikuwa akiwaonyesha watu nguvu kubwa ambayo Mungu alikuwa amempatia. Yesu alikuwa mwanadamu na Mungu alikuwa pamoja naye.

Katika Matendo ya Mitume 2:22 Petro anamwelezea kuwa  " Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua"

Na katika Johana 2:11 tunaambiwa: "Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini".

Hivi ndivyo Mungu alivyokusudia - watu walipoona miujiza na wakaamini maneno yake. Na kwa njia hii Bwana Yesu Kristo aliwafundisha watu kumpatia Mungu utukufu, maana ni Mungu aliyekuwa amempatia nguvu ya Roho Mtakatifu. Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.

FUNDISHO KWETU

Katika miujiza yote ambayo Bwana Yesu aliyofanya alikusudia kuwafundisha watu masomo maalumu. Na huo ndiyo muujiza wa kwanza alioufanya Yesu na muujiza huu ulifundisha somo muhimu sana. Mabarasi ya maji yalikuwepo kule " kwa desturi ya Wayahudi kwa ajili ya kutawadha " (mstari6). Maji yalikuwa ni kwa ajili ya kusafisha mwili. Maji yaliwawezesha kujisikia kuwa wako safi, lakini maji yasingeweza kumfanya mtu kuwa safi ndani, yaani akawa safi ndani ya moyo wake. Yesu alifundisha kwamba tunapaswa kuwa na "moyo safi”.

Maneno aliyosema Yesu yangeweza kumbadilisha mtu na kumfanya kuwa safi ndani. Wakati tunaposoma Neno la Mungu na kulitafakari na kulitunza katika mioyo yetu, hutubadilisha.

Basi, kila siku tulisome Neno naye Mungu atapendezwa kuona badiliko ndani yetu

Lugha ya Picha     

Ndani ya muujiza kwa hakika kuna idadi ya ishara ambazo tunaweza kuzitambua. Mabarasi sita ya maji yanazungumzia mwanadamu. Namba sita mara nyingi inahusiana na mtu na   muda huu   hatuta lizungumzia jambo hili. Haya mabarasi kwa namna yoyote ile  ni kwamba yalikuwa madogo; yalikuwa yenye ukubwa wa nzio mbili au tatu kwa maana  kuwa kila moja lilikuwa na uwezo wa kuchukua  ujazo wa galoni 25. Ni sawa na lita 113 kwa wale wanaotumia mfumo wa vipimo vya mita.  Mabarasi yalitengenezwa kwa mawe, yanaelezewa kuwa ni vyombo vya kutunzia maji. Hili ni neno ambalo linapatikana katika Maandiko Matakatifu  mara tatu; kwa mara ya kwanza lina patikana hapa, na lina patikana mara ya pili katika 2Wakorintho 3:3, na mwisho ni katika Ufunuo 9:20

 (2 Corinthians 3:3)  

Wanaume na wanawake wanapaswa kubadilika na kuwa “vibao vya mioyo ya nyama”. Nukuu katika Ufunuo inazungumzia kuhusu kutengeza vibao vya mawe kuwa sanamu. Kama Wayahundi walivyokuwa wamefanya. Walikuwa wamebadilisha (kugeuza) sheria za Mungu kuwa sheria za mwanadamu na desturi zao. Wazo la Wayahudi kuhusu dini kwa hakika ilikuwa ni: upotovu, desturi, falsafa isiyo na maadili ya Mungu, ambayo nguvu halisi na maana ya ibada ya kweli imezikwa. Na sasa imekuwa ni sanamu. Tahadhari ni kubwa hapa kwetu ndugu zangu wanaume na wanawake. Kwa uhakika ni kwamba, Bwana Yesu Kristo ataibadilisha mioyo ya wanaume na wanawake watakaokuwa wamempokea, kama vile aliyoweza kuyageuza maji yaliyo kuwa ndani ya yale mabarasi ya mawe.

Tunaona Bwana Yesu Kristo akiyabadilisha maji yaliyotumika kwa ajili ya desturi ya kutawadha (kunawa) na kuwa divai ya agano jipya.

Aliwaambia watumishi “Jalizeni mabalasi maji" nao walimtii, kama vile Mariamu alivyokuwa amewashauri. Basi, hapa, ulikuwa ni mfano wa kwanza wa kanuni ya ufuasi: “Lo lote atakalowaambia, fanyeni “.

Watumishi wakayajaliza mabarasi ya maji “hata juu”. Hili lilianzisha kanuni ambayo hautatokea kamwe upungufu wa tendo lile ambalo Yesu atatoa, uzima wa milele kwa watu wote ambao kwa mioyo yao watakaomwendea yeye.   Kwa kuwa Yesu atawapatia mahitaji yao, ili wasiwe na mahitaji tena ya jambo lolote. Maana Yesu kuwapatia sehemu yake yoyote kwa ajili ya uhitaji wa waamini ili kuwa huru mbali na dhambi, kupona magonjwa au madhaifu ya kibinadamu– na hata kuutoa uhai wake.

Mkuu wa meza alikuwa ni mtumishi wa bwana arusi ambaye aliwajibika kwa ajili ya utakaso au usafi na kuwapatia chakula wageni. Katika huduma yake tunaweza kutofautisha wajibu wa Kuhani Mkuu wa Israeli ambaye alikuwa na divai mpya, lakini asifahamu ilikotoka au ambaye aliigawa divai pasipo kujua kuwa divai ile ni bora kuliko ile ya zamani.

 (Waebrania 8:6)

“Tukio hili linatufaa sana sisi”, alisema, “yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu wote, wala lisiangamie taifa zima”.

Hakuwa bwana arusi wa duniani aliyeiweka divai iliyo njema mpaka sasa. Bali, alikuwa ni Mungu wa Israeli ambaye ulipotimia utimilifu wa wakati alimtuma Bwana arusi  wa mbinguni akiwa na divai ya kweli  ambayo  ndani  ina kiini cha uzima wa milele, ambayo mbele yake divai ya ( zamani) kale “ikaribu na kutoweka”.

Ingawa mkuu wa meza hakujua, lakini watumishi walifahamu kwa sababu walitii maneno ya Yesu na walitambua lile tukio na walishangaa sana. Lakini ishara ile ilikuwa ni kwa ajili ya wanafunzi wake ili utukufu wa Kristo udhihirishwe. Nguvu zake zilikuwa ni  za muhimu sana ili kuwathibitishia ukweli wa maneno yake, na kuwaondolea  desturi  yao ili waishikilie imani yao kwa ukamilifu. Kabla walikuwa wameamini mafundisho yake, na sasa alikuwa amewathibitishia ukweli na hata kwa dhamiri zao wakaamini na akawaandaa wakati huo ili pasipo mashaka yoyote wayaache mambo yao yote wamfuate yeye.

Mafundisho na Maonyo               

Kuna mafundisho makubwa yanayopatikana katika mwujiza huu mbele yetu. Tunahitaji ndugu wanaume na wanawake ili kuinywa “divai” ya mafundisho ya Yesu. Hii ina maana kwamba tufanye kila jitihada ili kuhakiksha kuwa watu wanashiriki “divai”. Tunatakiwa tuhakikishe kuwa tunahudhuria ili kusoma masomo ya kila siku. Tunapaswa kuhakikisha kuwa tunahudhuria vikao na mikutano yote inayofanyika katika jengo letu. Tunatakiwa tuhakikishe kuwa   chumba hakiwi tupo muda wa ibada bali kila mtu anakuwa tayari amekalia kiti chake. Ni lazima tuhakikishe kuwa tunakuwa na utaratibu wa kujifunza na kulitafakari Neno hilo. Tunapaswa  “tulitafakari  neno mchana na usiku”

Tujiulize sisi wenyewe kama tumekuwa sawa sawa na Masadukayo na Mafarisayo waliokuwepo wakati wa Yesu. Je, dini yetu ni upotofu?  Je, tunasingizia kuwa sisi ni watu wa dini, lakini wakati huo huo “tukiwa ni mbwa mwitu”?   Je, sisi ni wanafiki? Je, kama vile wengine wanavyoenenda katika mwenendo mbaya, ndivyo na sisi tunavyoenenda leo kama wao?  Je tumestarehe katika nafsi na roho, au ifahamike kuwa tuna ufahamu mdogo wa “Maziwa ya Akili” lakini ambayo yamekosa Divai?

Kusudi la mwujiza huu  kwa watu wale  ambao pasipo shaka  watajiita Israeli wa kiroho, basi waonyesha kuwa ikiwa tutakunywa “divai” ya  mafundisho yake, na kufunikwa na damu ya dhabihu yake, Bwana atakukuta katika huduma yake–  ni furaha kubwa itakayotimizwa kwenye utukufu wa  karamu ya arusi ya Mwanakondoo.

Na heri tuonekana kuwa tumestahili kuwepo kwenye arusi ya Mwanakondoo siku ile.

Swahili Title
ARUSI YA KANA Mwujiza wa kwanza wa Yesu
English files
Swahili Word file
Translator 1
Jonathan Nkombe
Literature type
English only